Mauaji, ubakaji na ghasia ziliwafanya maelfu kuzikimbia nyumba zao Colombia

Mauaji, ubakaji na ghasia ziliwafanya maelfu kuzikimbia nyumba zao Colombia

Shirikisho la kimataifa la chama cha msalaba mwekundu ICRC limesema mauaji, ubakaji na ghasia zilizopuuzwa wakati wa kampeni za uchaguzi wa Rais mwaka jana ziliwafanya maelfu kuzikimbia nyumba zao Colombia.

Jamii za watu wa asili na wale ambao chimbuko lao ni watumwa kutoka Afrika kwenye maeneo ya kusini na mwambao wa Pacific, ndio walioathirika vibaya kwa mujibu wa mwakilishi wa shirika la kuratibu misaada ya kibinadamu. ICRC na kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu wameorodhesha visa 800 vya ukiukwaji wa sheria za haki za kibinadamu mwaka jana na nyingi zinahusiana na mapigano baina ya jeshi, wanamgambo na waasi wa Marxist.

Watu 28 waliuawa, mashambulizi 61 dhidi ya raia na jamii na watu wengine 84 wametoweka. Pia vitisho vya amauaji vilitumika kuwashinikiza watu kuzikimbia nyumba zao. Takwimu rasmi zinaonyesha kwamba watu milioni 3.3 kati ya jumla ya watu milioni 46 wa nchi hiyo wamekuwa wakimbizi wa ndani kutokana na machafuko hayo, na ni wachache tuu waliothubutu kurejea makwao.