Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Juhudi kubwa zinahitajika ili kulinda afya za watu wa Afghanistan

Juhudi kubwa zinahitajika ili kulinda afya za watu wa Afghanistan

Afisa wa Umoja wa Mataifa leo ametoa wito wa kufanyika juhudi kubwa kuwasaidia Waafghanistan ambao wako katika hatari kutokana na majanga ya asili, vita na kutokuwepo kwa huduma za afya.

Dr Eric Laroche mkurugenzi msaidizi wa shirika la afya duniani WHO amesema juhudi kubwa zimefanyika kupanua wigo wa huduma za afya nchini humo lakini bado Waafghanistan wengi wanakabiliwa na hatari, na hatua za kuwalinda zinahitajika.

Dr Laroche amesema mambo yanayowakabili watu hao ni pamoja na majanga ya asili kama mafuriko, tetemeko la ardhi na vita. Amesema huduma za afya lazima ziimarishwe ikiwa ni pamoja na kuongeza idadi ya madaktari, wauguzi, wakunga na vifaa vya afya katika maeneo mengi ya nchi hiyo.