Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Rais Zuma kushirikiana na UNAIDS katika vita dhidi ya ukimwi Afrika ya Kusini

Rais Zuma kushirikiana na UNAIDS katika vita dhidi ya ukimwi Afrika ya Kusini

Mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na ukimwi UNAIDS Miche Sidibe alialikwa na serikali ya Afrika ya Kusini kwenye uzinduzi wa kampeni mpya ya upimaji wa ukimwi iliyoanzishwa na Rais Jacob Zuma.

Katika uzinduzi huo Rais Zuma ametangaza rasmi kuwa amepima na hana virusi vya HIV, hivyo anamchagiza kila mtu kupima na kujua hali yake. Bwana Sidibe amempongeza Rais Zuma na wizara ya afya ya Afrika ya Kusini kwa juhudi zao za kupambana na HIV.

Ameongeza kuwa hii ni kampeni kubwa kabisa ya kitaifa nchini humo tangu kumalizika kwa siasa za kibaguzi. Lengo kupima watu milioni 15 ifikapo mwishoni mwa mwaka 2011 ni hatua ya kihistoria.