WFP na mratibu wa masuala ya kibinadamu kusaidia waliokumbwa na njaa Niger

26 Aprili 2010

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limetangaza kuwa hivi sasa limeongeza mara mbili idadi ya watu linaowapa msaada wa chakula Niger.

Inawapa chakula watu milioni 2.3 wanaokabiliwa na njaa iliyosababishwa na ukame kwenye maeneo ya mashariki mwa Sahel. Mkurugenzi mkuu wa WFP amesema Niger imethirika vibaya na ukame na hivyo dunia inahitajika kuchukua hatua ili kuzuia athari mbaya zitakazotokana na baa la njaa.

Mratibu wa Umoja wa Mataifa wa masuala ya kibinadamu John Holmes yuko Niger ili kutathmini hali halisi na kuchagiza wahisani kutoa msaada wa dharura wa dola milioni 133 zaidi kunusuru maisha ya watu milioni 7.8 wanaokabiliwa na njaa. Elimia Casella ni msemaji wa WFP.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter