Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Upungufu wa fedha unatishia mapambano ya surua Afrika ya kati na magharibi

Upungufu wa fedha unatishia mapambano ya surua Afrika ya kati na magharibi

Nchini za Afrika ya magharibi na kati zimekumbwa na ugonjwa wa surua na kuwaathiri watoto zaidi ya 22,0000.

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limeonya kuwa upungufu wa fedha za kuendesha chanjo unatishia kuathiri juhudi za kupunguza vifo vya watoto wachanga. Upungufu wa dola milioni 16 za kuendesha kampeni ya chanjo ya marudio unatishia afya za watoto Afrika zikiwemo nchi 16 ambazo zimekumbwa na mlipuko wa ugonjwa huo hivi karibuni.

Katika nchi za Afrika ya magharibi na ya kati ni asilimia 80 tuu au chini ya hapo ambao wamepata chanjo. Hicho ni kiasi kidogo kuliko mapendekezo ya shirika la afya duniani WHO ya asilimia 95 kupata chnjo. Karibu vifo 200 vya watoto vitakanavyo na surua vimeripotiwa katika nchi 16 zilizokumbwa na ugonjwa huo kwa mwaka jana.