Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Yameundwa chombo kipya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira

Yameundwa chombo kipya kukabiliana na uchafuzi wa mazingira

Mkutano wa kwanza wa bodi iliyoundwa mwaka 2003 ya Kiev Protocol kuhusu uchafuzi wa mazingira PRTR umemalizika mjini Geneva.

Moja ya mambo waliyotoka nayo kweny mkutano huo ni uundwaji wa chombo kipya cha kimataifa kitakachohakikisha taarifa muhimu za tishio la uharibifu wa mazingira kutokana na taka za sumu zinapatikana.

Kwa mujibu wa katibu mkuu wa UNECE Jan Kubis chombo hicho ni muhimu sana kwani kitasaidia kulinda sio tuu mazingira bali maisha ya watu kutodhuriwa na taka hizo za sumu.