Skip to main content

Mwakilishi mpya wa UM nchini Burundi amewasili kuanza kazi

Mwakilishi mpya wa UM nchini Burundi amewasili kuanza kazi

Mwakilishi maalumu mpya wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Burundi amewasili ili kuanza shughuli zake. Mwakilishi huyo balozi Charles Petrie ana jukumbu kubwa la kuhakikisha kuwa uchaguzi mkuu unaoanza mwezi ujao unakuwa huru, wa utulivu na wa haki.

Hata hivyo itakuwa ni kibarua kigumu kwa mwakilishi huyo kwani Burundi ilikwisha watimua nchini wawakilishi watatu wa umoja wa Mataifa katika kipindi cha miaka mitano. Kutoka Bujumbura mwandishi wetu Ramadhan Kibuga anaarifu zaidi: