Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Burundi inajiandaa na uchaguzi mkuu na mjumbe wa UM ameshawasili nchini humo

Burundi inajiandaa na uchaguzi mkuu na mjumbe wa UM ameshawasili nchini humo

Wakati wananchi wa Burundi wakiendelea na maandalizi ya uchaguzi utakaoanza hivi karibuni, mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa balozi Charles Petrie amewasili nchini humo.

Pamoja na kusimamia shughuli za mashirika ya Umoja wa Mataifa Balozi Petrie atakuwa na jukumu la kuhakikisha nchi hiyo inafanya uchaguzi ulio huru, haki na wa utulivu.

Mwandishi wetu Ramadhan kibuga akiwa Bujumbura anaarifu zaidi.