Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Uwepo wa makundi ya wanamgambo wenye silaha kunatishia hatua za amani Lebanon

Uwepo wa makundi ya wanamgambo wenye silaha kunatishia hatua za amani Lebanon

Ripoti ya Umoja wa Mataifa imeonya kuwa licha ya juhudi za kuipa nguvu serikali ya Lebanon na mipaka yake, uwepo wa makundi ya wanamgambo wenye silaha unatishia amani ya nchi hiyo na ukanda mzima.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akiandika katika ripoti yake kuhusu utekelezaji wa azimio namba 1559 amesema kuendelea kuwepo kwa makundi ya wanamgambo wenye silaha nje ya serikali kunatishia demokrasia na amani ya watu wa Lebanon, na pia ni kikwazo cha maendeleo.

Ameongeza kuwa mbali ya kuwanyima haki watu wa Lebanon pia makundi hayo yanatishia usalama wa ukanda mzima. Amesema makundi hayo yanatakiwa kuheshimu serikali, uhuru na demokrasia ya watu wa Lebanon.