Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kuchukua mtazamo mpya kuwasaidia watu kaskazini mwa Uganda

WFP kuchukua mtazamo mpya kuwasaidia watu kaskazini mwa Uganda

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limesema linabadili mtazamo wa jinsi linavyoendesha shughuli zake katika jimbo la Karamoja linalokabiliwa na ukame kaskazini mwa Uganda.

WFP inasema katika hatua inazochukua ni pamoja na kuzindua operesheni za dharura wiki ijayo sambamba na mpango mpya utakaosaidia kukabiliana vyema na chanzo cha upungufu wa chakula na utapia mlo.

Mpango huo wa dharura una lengo la kuwafikia watu laki tatu wanaokabiliwa na matatizo ya chakula kwa kuwagawia mgao wa mwezi mmoja wa chakula. Eneo la Karamoja limekuwa likikumbwa na matatizo ya chakula mara kwa mara kutokana na ukame uliokithiri.