Mwakilishi wa UM amesema hofu kubwa ya MONUC DRC ni kuwalinda raia

Mwakilishi wa UM amesema hofu kubwa ya MONUC DRC ni kuwalinda raia

Mwakilishi maalumu wa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Alan Dos ametembelea eneo la Mbandaka na kukutana na viongozi mbalimbali wa serikali . Akiwa huko kusema hofu ya mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo ni ulinzi wa raia.

Doss aliambatana na kamanda mkuu wa MONUC na naibu mkurugenzi wa masuala ya kisiasa. Lengo la ziara yao ni kuwahahikishia watu wa jimbo la Equateur faraja na mshikamano wa MONUC baada ya shambulio lililofanyika tarehe 4 na 5 mwezi huu.

Pia amezungumza na uongozi wa jimbo akiwepo gavana, na kamanda wa jeshi la eneo hilo, mashirika yasiyo ya kiserikali na wafanyakazi wa Umoja wa Mataifa na kusema hivi sasa kikosi cha MONUC kitaimarishwa zaidi.