Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tuzo ya kinara wa dunia mwaka huu imelenga uchumi unaolinda mazingira

Tuzo ya kinara wa dunia mwaka huu imelenga uchumi unaolinda mazingira

Tuzo ya kinara wa dunia mwaka 2010, tuzo ambayo ni ya juu kabisa ya Umoja wa Mataifa kwa viongozi bora wanaojali mazingira imetolewa na washindi wametangazwa leo mjini Seoul Korea ya Kusini.

Washindi wa mwaka huu ni sita na wamepatikana kutoka sehemu na nyanja mbalimbali kama serikalini, sayansi, biashara na burudani, na kila mmoja ameweza kuonyesha ni jinsi gani kuchukua hatua, kuwa na ari, kujitolea na kuwa mbunifu kunaweza kusaidia kupunguza kiwango cha gesi ya cabon na kuwa na uchumi unaozingatia mazingira katika karne hii ya 21.

Washindi hao wanatoka Afghanistan, Uchina, Guyana, India, Japan na Maldive. Washindi hao wamekabidhiwa tuzo zao na mkurugenzi mkuu wa shirika la Umoja wa mataifa la mazingira UNEP Achim Steiner katika siku hii ya kimataifa ya kuilinda na kuienzi dunia.