Leo ni Siku ya Kimataifa ya kuenzi dunia lakini dunia ipo katika shinikizo: Ban

22 Aprili 2010

Leo ni Siku ya Kimataifa ya kuienzi na kuithamini dunia. Mwaka jana mkutano mkuu wa Umoja wa Mataifa uliamua kuwa tarehe 22 April itakuwa siku ya kuienzi dunia mama kwa kuonyesha umuhimu uliopo wa kutegemeana baina ya binadamu, viumbe vingine na dunia.

Ban ameongeza kuwa kuilinda dunia ni lazima iwe moja ya mikakati ya kutimiza malengo ya milenia. Siku ya kuienzi na kuithamini dunia ilianza kuadhimishwa mara ya kwanza miaka 40 iliyopita.

 

♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter