Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Kumbukumbu ya chernobyl inakumbusha changamoto za mazingira

Kumbukumbu ya chernobyl inakumbusha changamoto za mazingira

Zimesalia siku chache tuu kabla ya kumbukumbu ya miaka 24 ya zahma ya kinu cha nyuklia cha Chernobyl Ukraine iliyokatili maisha ya watu zaidi ya laki tatu.

Mkutano wa kila mwaka wa afya na mazingira unajadili suluhu ya changamoto za mazingira kama mabadiliko ya hali ya hewa, na kuwa mazingira yenye sumu na athari za baada ya zahma ya Chernobyl. Mkutano huo umeandaliwa na World Information Transfer Society,ambayo imekuwa mfadhili wa Ukraine tangu mwaka 1992 .

Balozi wa Ukraine kwenye Umoja wa Mataifa Yuriy Sergeyev amewakumbusha washiriki wa mkutano kuwa mripuko wa 1986 katika kinu cha nyuklia cha Chernobyl umekuwa janga la kitaifa kwa nchi yake , ambayo mpaka sasa inakabiliana na athari za kiuchumi na kijamii.

Kumbukumbu ya miaka 24 ni kukumbusha ukubwa wa tatizo hilo na athari zake sio tuu kwa Ukraine. Watu zaidi ya lakitatu waliuawa na wengine wengi wanasumbuliwa na saratani hadi sasa. Balozi huyo amesema ni wakati wa kushirikiana kwa pamoja kuhakikisha tukio kama hilo halitokei tena.