Mfuko wa UM kushirikiana na American Idol katika kipindi malumu

21 Aprili 2010

Mamilioni ya watazamaji wa kipindi maarufu cha televisheni cha mashindano ya kuimba hapa Marekani American Idol watapata fursa usiku wa leo kuchangia katika shughuli za mfuko wa Umoja wa Mataifa UNF duniani kote.

Shughuli hizo ni pamoja na kusaidia kuijenga upya Haiti baada ya tetemeko la ardhi na hata kuwasaidia kuwawezesha wanawake na wasichana nchini Ethiopia.

Kipindi cha leo cha American Idol walichikiita Idol gives Back kitahusisha burudani kutoka kwa miongoni mwa waigizaji na waimbaji maarufu wa Hollywood. Katika miaka iliyopita kipindi hicho kilimuhusisha Rais wa Marekani Barack Obama, waziri mkuu wa uingereza Gordon Brown, mcheza sinema maarufu Brad Pitt mwimbaji maarufu Mariah Carey na watu wengine mashuhuri.

Pamoja na UNF mashirika mengine ya kujitolea kama Children Health Fund, feeding America, na Save the children yamechaguliwa kufaidika na fedha zitakazokusanywa mwaka huu.

Vipindi vilivyopita vya Idol Gives Back vimekusanya dola milioni 140 kusaidia mambo mbalimbali Marekani na kwingineko duniani na watazamaji mwaka huu wanachagizwa kuwashawishi rafiki zao kuchangia kupitia wavuti kama twitter na facebook.

 

♦ Kurambaza ukurasa mahsusi wa Siku ya Kiswahili Duniani bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter