Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO inatoa msaada kwa wafugaji wa Afrika ya Magharibi

FAO inatoa msaada kwa wafugaji wa Afrika ya Magharibi

Shirika la chakula na kilimo FAO limesema linaongeza msaada wake kwa wakulima na wafugaji nchini Niger na Chad kutokana na tatizo la chakula lililosababishwa na msimu duni wa mvua.

Mvua hizo ambazo hazikunyesha ipasavyo zimesababisha kuwa na mavuno hafifu na kukausha chakula cha mifugo. Watu takribani milioni 9.8 wako katika hatari ya baa la njaa katika nchi hizo mbili.

Nchi jirani za Burkina Faso na Mali maeneo yake ya kaskazini yamearifiwa kuwa maelfu ya mifugo inakabiliwa na upungufu wa chakula. FAO inasema la muhimu kwa sasa ni kupata chakula cha mifugo na kuwagawia wakulima mbegu kwa ajili ya msimu ujao wa kupanda.