Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalaumu wa UM kuhusu usafirishaji haramu wa watu amemaliza ziara yaki Misri

Mtaalaumu wa UM kuhusu usafirishaji haramu wa watu amemaliza ziara yaki Misri

Mtaalamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu usafirishaji haramu wa watu hususani wanawake na watoto Joy Ngozi Ezeilo amehitimisha ziara yake nchini Misri.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Cairo Ezeilo amesema ameiangalia mifumo yoye ya usafirishaji haramu wa watu nchini humo na kutathimini hatua zilizopigwa na serikali ya Misri kukabiliana na tatizo hilo.

Amebaini kuwa usafirishaji haramu hasa wa wasichana wenye umri mdogo kwa ajili ya biashara ya ngono, ndoa za muda mfupi, kutumikishwa katika kazi na biashara ya ukahaba upo kwa kiasi kikubwa.