Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baadhi ya nchi zimeanza kuonyesha matumaini ya kupunguza gesi ya cabon: UNEP

Baadhi ya nchi zimeanza kuonyesha matumaini ya kupunguza gesi ya cabon: UNEP

Utafiti wa kuangalia upunguzaji wa gesi ya cabon katika ukuaji wa uchumi umebaini kuwa licha ya sintofahamu inayoghubika majadiliano ya kimataifa ya mabadiliko ya hali ya hewa kuna nchi zimepiga hatua kupunguza gesi ya cabon.

Utafiti huo ulioandaliwa na shirika la Umoja wa Mataifa linalohusika na mazingira UNEP umehitimisha kwamba katika robo ya kwanza ya mwaka huu wa 2010 nchi 32 zimepiga hatua kubwa katika kupunguza matumizi ya cabon.

Nchi zimeonekana kuwa mfano ni pamoja na Ujerumani, Uchina na Jamuhuri ya watu wa Korea. Lakini India, Indonesia, Kenya, Mexico, Uphilipino na Rwanda pia zimepiga hatua katika masuala ya hali ya hewa tangu kumalizika kwa mkutano wa Copenhagen.