Skip to main content

Mwandishi mwingine wa habari auawa Honduras UNESCO yalaani vikali

Mwandishi mwingine wa habari auawa Honduras UNESCO yalaani vikali

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la sayansi, elimu na utamaduni UNESCO amelaani vikali mauaji ya mwandishi habari mwingine nchini Honduras.

Mkuu wa UNESCO Irina Bokova akilaani mauaji hayo amesema anatumai serikali itachunguza na kuchukua hatua zinazostahili kwa wahusika. Ameongeza kuwa ni muhimu kwa wafanyakazi wa vyombo vya habari nchini humo kuweze kutimiza haki yao ya uhuru wa kujieleza bila kuhofia maisha yao.

Shirika la kimataifa la waandishi wa habari wasio na mipaka limesema mauji ya Hernandez yanafanya idadi ya waandishi habari waliouawa Honduras mwaka huu pekee kufikia sita.