Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mpango wa chanjo ya polio Afrika Magharibi waathirika kutokana na adha ya usafiri

Mpango wa chanjo ya polio Afrika Magharibi waathirika kutokana na adha ya usafiri

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF na shirika la afya duniani WHO wamesema mpango wao wa chango ya polio kwa nchi 19 Afrika ya magharibi umeathirika kutokana na kusitishwa kwa safari za ndege kutoka Ulaya.

UNICEF inasema dozi milioni 15 za chanjo ya polio zimekwama barani Ulaya na kusababisha chanjo hiyo kuahirishwa Sierra Leone na Burkina Faso. Kampeni hiyo ya pamoja ina lengo la kuwapa chanjo watoto milioni 95 walio na umri wa chini ya miaka mitano. Dawes anasema hata hivyo hatua zimepigwa katika chanjo hiyo