Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Zaidi ya wiki tangu volkano ya Eyjafjalla kulipuka tathmini ya athari yafanyika

Zaidi ya wiki tangu volkano ya Eyjafjalla kulipuka tathmini ya athari yafanyika

Kitengo cha Umoja wa Mataifa kinachohusika na kupunguza athari za majanga na jumuiya ya Ulaya ya masuala ya volkano wamezungumza na waandishi wa habari mjini Geneva kuhusu athari za volkano nchini Iceland.

Rais wa jumuiya ya Ulaya ya masuala ya volkano Henry Gaudru amesema volkano ya Iceland ni ndogo ikilinganishwa na volkano zingine za hivi karibuni kama Pinatubo. Amesema kilichofanya volkano ya Iceland kuwa na uzito mkubwa ni moshi mzito ambao unaelekea Ulaya na kusababisha tafrani katika usafiri wa anga.

Amesema ni salama kusafiri kwa sasa lakini akaongeza kuwa ni jukumu la kila nchi kuhakikisha usalama wa ndege zinazosafiri.