Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

\Mahakama ya kimataifa ya haki imetoa uamuzi kuhusu mzozo wa kiwanda cha karatasi baina ya Argentina na Uruguay

\Mahakama ya kimataifa ya haki imetoa uamuzi kuhusu mzozo wa kiwanda cha karatasi baina ya Argentina na Uruguay

Mahakama ya kimataifa ya haki leo imetoa uamuzi wa kesi iliyowasilishwa na Argentina dhidi ya Uruguay mwaka 2006 ikidai uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na kiwanda cha karatasi kilichoko mpakani mwa nchi hizo mbili.

Mahakama imebaini kwamba Uruguay ilikiuka jukumu lake la kuiarifu Argentina mipango yake ya kujenga viwanda viwili vya karatasi katika mto Uruguay kabla ya idhini ya ujenzi huo kama inavyotakiwa kwenye mkataba wao wa 1975 unaoangalia matumizi ya mto huo.

Lakini hata hivyo mahakama hiyo imeyakataa madai ya Argentina ya kutaka kulipwa fidia kwa sababu haina ushahidi unaothibitisha kwamba mabaki ya moja ya viwanda hivyo ambacho kilianza 2007, kimeharibu ubora wa maji au mfumo wa matumizi ya maji hayo.

Kwa miaka mitatu sasa Wargentina wanaopinga kiwanda hicho wamekuwa katika kampeni huku, wakifunga daraja kubwa la mto huo.