Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP kupeleka chakula zaidi kuwasaidia waathirika wa tetemeko Haiti

WFP kupeleka chakula zaidi kuwasaidia waathirika wa tetemeko Haiti

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP linasambaza mgao wa chakula kwa watu milioni mbili kila siku, chakula hicho ni pamoja na ambacho kiko tayari, pia inatoa tani 1000 za bisikuti katika maeneo 30 katika maandalizi ya msimu wa mvua na kimbunga.

WFP inasema tayari ina tani 35,000 na vitu mchanganyiko vinavyoweza kuwalisha watu milioni 1.3 kwa wiki sita.Pia inasaidia katika kuwahamisha wakimbizi wa ndani mjini Port-au-Prince kabla ya mvua kuanza.

Mpango wa fedha kwa chakula sasa umepanua wigo na wanatarajia maelfu ya wafanyakazi watafaidika na mpango huo kama anavyofafanua msemaji