Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

WFP imeukaribisha ufadhili wa Ulaya utakaosaidia Ethiopia

WFP imeukaribisha ufadhili wa Ulaya utakaosaidia Ethiopia

Shirika la mpango wa chakula duniani WFP limeshukuru na kupongeza mchango wa mamilioni ya dola uliotolewa na tume ya Ulaya. Msaada huo wa dola milioni 23 umetolewa na tume ya Ulaya kupitia kitengo maalumu cha msaada wa kibinadamu ECHO.

Msaada huo ni kwa ajili ya kusaidia watu takribani milioni 2.3 nchini Ethiopia wanaohitaji msaada wa chakula. Ethiopia imekuwa ikikabiliwa na matatizo ya njaa kila wakati na WFP imekuwa msitari wa mbele kutoa msaada.

WFP inasema msaada huo utasaidia sana kuokoa maisha ya watu waalio katika hali mbaya nchini humo.