Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNICEF inajiandaa kuwasaidia maelfu ya wanafunzi walioathirika na tetemeko Uchina

UNICEF inajiandaa kuwasaidia maelfu ya wanafunzi walioathirika na tetemeko Uchina

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF limesema kutokana na ombi la serikali ya Uchina linajiandaa kupeleka msaada kwa maelfu ya wanafunzi walioathirika na tetemeko la ardhi.

Kwa mujibu wa uongozi wa eneo lililokumbwa na tetemeko, asilimia 80 ya shule za msingi na asilimia 50 ya shule za sekondari mjini Yushu zimebomolewa na kuathiri wanafunzi zaidi ya elfu 20 na walimu zaidi ya 900.