Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imesema imesikitishwa na hatua ya Australia ya kuwaweka kizuizini wanaoomba hifadhi

UNHCR imesema imesikitishwa na hatua ya Australia ya kuwaweka kizuizini wanaoomba hifadhi

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limeelezea kusikitishwa kwake na kushindwa kwa serikali ya Australia kutafuta njia nyingine badala ya kuwaweka mahabusu watu wanaoomba hifadhi ya ukimbizi.

UNHCR inasema watu hao wanawasili na boti nchini humo na hawatoi tishio lolote la afya au usalama. Katika taarifa yake iliyotolewa mjini Canbera UNHCR inasema wazi kupinga hatua hiyo ya kuwaweka mahabusu waomba hifadhi.

Taarifa hiyo inasema uzoefu unaonyesha kwamba hatua kama hizo zinaweza kuwa na athari za kiafya na maisha ya watu na hususani ambao tayari wameshapitia mateso na adha kubwa kabla ya kuwasili nchini humo. Serikali ya Australia wiki iliyopita ilitangaza kusitisha maombi ya ukimbizi kwa Waafghanistan na Wasri Lanka wanaowasili kwa boti nchini humo.