Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ili kukabiliana na ubakaji wanajeshi wa kulinda amani wasalie DR Congo

Ili kukabiliana na ubakaji wanajeshi wa kulinda amani wasalie DR Congo

Wanajeshi wa Umoja wa Mataifa wasalie Congo DRC amesema afisa mwandamizi wa Umoja wa Mataifa na ameonya kuwa juhudi za kukabiliana na ubakaji Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo zitakuwa ngumu ikiwa wanajeshi wa kulinda amani wataondolewa nchini humo.

Akizungumza katika ziara yake nchini humo mjumbe huyo maalumu kuhusu unyanyasaji wa kimapenzi katika maeneo yenye migogoro Magort Wallstrom amesema wanajeshi wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa MONUC wamewapa wanawake wa Congo matumaini ya kuendelea na majukumu yao ya kila siku.

Inakadiriwa kuwa maelfu ya wanawake hubakwa kila mwaka na wanajeshi wa serikali na makundi ya waasi nchini humo. Rais Joseph Kabila wan chi hiyo amesema anataka wanajeshi wa Umoja wa Mataifa kuondoka Congo ifikapo mwisho wa Juni mwakani.