Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mtaalamu wa UM amesifu sheria ya Uingereza ya kushughulikia wanaofaidika na mikopo

Mtaalamu wa UM amesifu sheria ya Uingereza ya kushughulikia wanaofaidika na mikopo

Mtaalamu wa haki za binadamu wa Umoja wa Mataifa kuhusu madeni ya nje ,leo amepongeza sheria ya Uingereza ya afueni ya madeni.

Sheria hiyo inazuia kiwango cha uwezo wa kuchukua fedha zaidi kwa kile kinachojulikana kama fedha za mdeni na kuweza kuzishitaki nchi masikini katika mahakama kwa ajili ya kulipwa madeni , akitoa ushahidi wa hukumu ya hivi karibuni iliyoihusisha Liberia.

Mtaalamu huyo Cephas Lumina amesema sheria hii ni mara ya kwanza kwa nchi kuzuiwa kufaidika na fedha za mkopo. Katika wajibu wake kama mtaalamu binafsi wa Umoja wa Mataifa kwa athari za madeni ya nje na masuala mengine ya kimataifa yanayohusiana na majukumu ya kifedha, ni kuhakikisha haki za binadamu zinatekelezwa, hasa katika masuala ya kiuchumi, kijamii na kiutamaduni.

Amesema anaipongeza Uingereza kwa kuchukua hatua hiyo kuzuia watu wanaofaidika kwa kupitia migongo ya raia wa nchi wanazozidai na fedha za walipa kodi wa nchi zinazounga mkono afueni ya madeni. Mkopo huo huwa unanunua madeni yote au sehemu ya madeni ya nchi masikini. Na mara nyingi huwa wanazilenga nchi ambazo zimefutiwa madeni na kisha wanazishitaki ili kulipa madeni hayo , na kuchukua fedha ambazo ambazo nchi hizo zimebakiwa nazo baada ya kufutiwa madeni.