Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Amri za jeshi la Israel huenda zikakiuka sheria za kimataifa na haki za binadamu

Amri za jeshi la Israel huenda zikakiuka sheria za kimataifa na haki za binadamu

Mtaalamu binafsi wa Umoja wa Mataifa wa haki za binadamu katika eneo linalokaliwa la Palestina ameonya kuwa amri mbili zilizotolewa na jeshi la Israel huenda zikakiuka sheriia za kimataifa za masuala ya kibinadamu na haki za binadamu.

Richard Falk amesema amri hizo zinaonekana kuwawezesha wa Israel kuwashikilia, kuwafungulia mashitaka, kuwafunga na au kurejesha kwa nguvu mtu yeyote au watu wote walioko Ukingo wa Magharibi. Amesema kuwarejesha kwa nguvu chini ya amri mpya kutafanyika bila kutathimini mambo ya kisheria.

Amesema kwa kufanya hivyo hawaheshimu haki za watu wanaoishi katika eneo hilo linalokaliwa kwa kulinda maslahi wa wanaolikalia na kwamba jambo hilo linahitaji kuangaliwa kisheria kwa kila nyanja lakini pia wajibu ilionao Israel katika kifungu namba 49 cha mkataba wa nne wa Geneva unaosema huwezi kuwarejesha kwa nguvu watu walioko katika eneo linalokaliwa.

Bwana Falk amesema ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu za kimataifa na na sheria za kimataifa za masuala ya kibinadamu vinaweza kuhusishwa na vitendo vinavyofanywa na serikali ya Israe chini ya amri hizo. Ameonya kwamba ukiukaji huu unaweza kuwa na athari kubwa kwamba vijana wanakuwa wahanga wa amri hizo.