Skip to main content

Maelfu ya watu Darfur Sudan hawana msaada wa maji, chakula na madawa

Maelfu ya watu Darfur Sudan hawana msaada wa maji, chakula na madawa

Mratibu wa Umoja wa mataifa wa masuala ya kibinadamu nchini Sudan George Charpentier amesema machafuko yanayoendelea mashariki mwa Jebel Marra kwenye jimbo la Darfur yanaleta adha kubwa kwa raia.

Amesema kwa sasa inakuwa vigumu kwa mashirika ya misaada kuyafikia maeneo hayo ambayo kwa miaka mitano yamekuwa yakipata msaada wa chakula maji na madawa.

George amesema operesheni zao zimelazimika kusitishwa kwa wiki kadhaa sasa ambapo wamekuwa wakijitahidi kuwafikia raia katika maeneo ya milimani ili kutathimini hali halisi na kuwapa msaada wowote unaohitajika, lakini hilo limeshindikana. Ameongeza kuwa cha muhimu hivi sasa ni kuweza kuyafikia maeneo hayo ili kuwanusu watu wanaohitaji msaada wa haraka.