Balozi Mwema wa UNHCR ametoa wita wa kuwalinda raia nchini Somalia

Balozi Mwema wa UNHCR ametoa wita wa kuwalinda raia nchini Somalia

Mwigizaji maarufu wa filamu ambaye pia ni balozi mwema wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Angelina Jolie ameelezea hofu yake juu ya usalama na maisha ya maelfu ya wakimbizi wa ndani waliokwama Mogadishu Somalia.

Watu takribani 170,00 wamelazimika kuzikimbia nyumba zao nchini humo tangu mwanzo wa mwaka huu. Mamia wameuawa, na wengine wengi kujeruhiwa katika machafuko ya karibuni mjini Mogadishu. Wengi wamekuwa wakimbizi wa ndani na wengine hawana njia yoyote ya kutoka nchini humo.