Ban ameelezea hofu yake juu ya matatizo yanayowakabili watu wa asili
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon akizungumza katika kikao cha tisa cha hali ya watu wa asili asubuhi ya leo ,amesema anahofia matatizo yanayowakabili watu hao.
Ban amesema ripoti ya Umoja wa Mataifa iliyotoka Januari mwaka huu kuhusu hali ya watu wa asili inasema watu hao wanakabiliwa na matatizo mengi na makubwa kama umasikini,matatizo ya afya, uhalifu na ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu duniani kote.
Watu hao ni asilimia tano ya idadi ya watu duniani, lakini ni theluthi moja ya watu wote masikini duniani. Ameonya kwamba kutokana na makisio ya hivi sasa asilimi 90 ya lugha zote zitatoweka katika kipindi cha miaka 100.
Na kutoweka kwa lugha hizi kunaondoa kipengele maalumu cha uasilia wa kundi Fulani. Ban ametikata serikali zote, watu wa asili, mfumo wa Umoja wa Mataifa na wadau wengine wote kuhakikisha kwamba mtazamo wa azimio la haki za watu wa asili unatimizwa kwa wote.