Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID imewasiliana na baadhi ya askari wake waliotekwa nyara Sudan

UNAMID imewasiliana na baadhi ya askari wake waliotekwa nyara Sudan

Mpango wa pamoja wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa afrika Darfur nchini Sudan UNAMID umefanya mawasiliano na baadhi ya askari wake nne waliotekwa nchini Sudan.

Wanajeshi hao wanne ambao ni kutoka afrika ya Kusini walitoweka kwenye kituo chao cha Nyala saa za alasiri Jumapili iliyopita. Msemaji wa UNAMID Kemal Saiki ameiambia Radio ya Umoja wa Mataifa kwamba watu wanaowashikilia wanajeshi hao wamewasiliana na UNAMID kwa njia ya simu.

Amesema "wametuarifu kwamba watu hao wako katika hali nzuri.Hawakutupa taarifa zaidi za wapi walipo ila tuu kwamba wako salama,. Kilicho cha muhimu ni kwamba tuna ushahidi kuwa wako hai. Kemal Saiki amesema hafahamu lolote kuhusu madai ya kikombozi yaliyotolewa na watekaji hao kwenye vyombo vya habari. Amesema UNAMID inachotaka ni kurejea kwa wenzao wakiwa salama na haraka iwezekanavyo.