Skip to main content

Mkutano wa kimataifa wa utabiri wa hali ya hewa umemalizika Nairobi

Mkutano wa kimataifa wa utabiri wa hali ya hewa umemalizika Nairobi

Mkutano wa kimataifa wa utabiri wa ya hali ya hewa ulianza tarehe 12 April mjini Nairobi nchini Kenya umehudhuriwa na watu mbalimbali.

Mkutano huo uliandaliwa na shirika la kimataifa la utabiri wa hali ya hewa WMO kwa mwaliko rasmi wa serikali ya Kenya na uliwahusisha mawaziri wa hali ya hewa kutoka kote barani Afrika, Umoja wa Afrika, Bank ya dunia, Umoja wa Ulaya na nchi kadhaa za mabara mengine.

Mkutano huo ni wa kwanza kufanyika barani Afrika na lengo lake lilikuwa kuzishawishi serikali kutilia maanani ripoti zinazotolewa na mashirika ya utabiri wa hali ya hewa ili kukabiliana na athari zitokanazo na mabadiliko ya hali ya hewa. Mwandishi wetu wa Nairobi Jason Nyakundi ameufuatilia kwa karibu mkutano huo na anatufahamisha yaliyojiri kwa juma zima mkutanoni katika makala hii, ungana naye.