Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon amesema amani lazima ijengeke akilini na mioyoni mwa watu

Ban Ki-moon amesema amani lazima ijengeke akilini na mioyoni mwa watu

Katibu Mkuu wa Umoja wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon leo amesisitiza kwamba haja ya raia wa nchi inayotoka katika vita ni kuona faida ya kurejea kwenye amani.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa alikuwa akizungumza katika mkutano wa baraza la usalama uliokuwa ukijadili mikakati ya kujenga upya amani baada ya vita. Mkutano huo umehudhuriwa na mwaziri wa mambo ya nje kutoka nchi mbalimbali. Amesisitiza  haja ya kuchukua mtazamo thabiti wa kurejesha amani kwa kushughulikia mambo muhimu ya kisiasa, kiuchumi na kijamii ambayo yanasaidia kuleta amani.

Amesema tunajenga amani katika mawazo na mioyo ya watu. Hii ina maana kuondoa tofauti zilizopo zinazowagawa watu. Amani haitodumu hadi tuu watu watakapoona faida yake katika maisha yao ya kila siku, usalama, haki, ajira na matarajio ya maisha bora ya baadaye. Na kwa maana hii kazi yetu lazima ziku zote ifuate muongozo wa matakwa ya taifa."

Bwana Ban ametangaza kwamba mwezi huu mfuko wa kujenga amani utafikia dola milioni 200 unazotoa kama msaada. Amesema wahisani 48 na karibu dola milioni 350 za ahadi na zilizopo, mfuko huo unaendelea kupiga hatua na amewaomba wahisani kuongeza msaada wao.