Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

ICRC imethibitisha kuachiliwa huru wafanayakazi wake wanane Congo DRC

ICRC imethibitisha kuachiliwa huru wafanayakazi wake wanane Congo DRC

Kamati ya kimataifa ya chama cha msalaba mwekundu ICRC imethibitisha kuachiliwa huru kwa wafanyakazi wake wanane walitokekwa tangu tarehe 9 April na kundi la wanamgambo wenye silaha Kivu ya Kusini nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Wafanyakazi saba ambao ni raia wa Congo na mmoja Mswis walitekwa baada ya kumaliza tathimini ya mahitaji ya wakimbizi wa ndani katika eneo hilo. ICRC inasema wanafanyakazi hao wameachiliwa leo Ijumaa katika eneo la Fazi na kukabidhiwa kwa chama hicho kilichokuwa kikipata msaada wa kiufundi kutoka kwa mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa nchini humo MONUC.

ICRC inasema imefurahi kurejeshewa wafanyakazi wake na imewashukuru wote waliosaidia kufanikisha hatua hiyo.