Skip to main content

Ingawa mafua ya ndege yamedhibitiwa kwa kiasi kikubwa bado ni tishio duniani

Ingawa mafua ya ndege yamedhibitiwa kwa kiasi kikubwa bado ni tishio duniani

Afisa wa Umoja wa Mataifa amesema ingawa juhudi za kimataifa zimefanikisha kutokomeza homa ya mafua ya ndege ya H5N1 kutoka kwa kuku karibu kwa nchi zote 63 zilizoathirika na mlipuko wa ugonjwa huo 2006 bado homa hiyo ipo.

Wataalamu walihofia huenda ingekuwa mbaya zaidi na kusababisha vifo vingi ingeanza kuambukiza kwa kupitia binadamu. Lakini hofu sasa imehamia kwenye mafua mengine H1N1 yanayojulikana kama mafua ya nguruwe. Mafua ya nguruwe yameathiri Misri, Indonesia, Bangladesh, Vietnam na Uchina.