Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mkuu wa Haki za Binadamu ametaka kusitishwa mauaji Gaza

Mkuu wa Haki za Binadamu ametaka kusitishwa mauaji Gaza

Kamishina Mkuu wa Umoja wa Mataifa wa Haki za Binadamu Navi Pillay leo ameutolea wito uongozi wa Gaza kusitisha mauaji na kufuta hukumu ya kifo.

Usiku wa tarehe 14 na 15 mwezi huu wafungwa wawili wanaoshutumiwa kwa makosa yanayohusiana na Israel kuikalia Palestina walinyongwa Gaza.

Pillay amesema ametiwa hofu sana na mauaji hayo na uwezekano kwamba wengine pia wanaweza kuuawa hivi karibuni. Tarehe 24 Machi uongozi uliojitenga wa Gaza ulitangaza hadharani uamuzi wa kuwanyonga watu kadhaa wanaodaiwa kuwa wahalifu. Na siku nne baadaye wakatangaza kwamba mchakato wa kupitisha sheria ya hukumu hiyo ya kifo umeanza.