Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNHCR imelaani mauaji ya raia yanayoendelea nchini Somalia

UNHCR imelaani mauaji ya raia yanayoendelea nchini Somalia

Shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR limelaani vikali vitendo vya kuwafanya raia wahanga wa machafuko yanayoendelea Somalia.

Shirika hilo linasema limeshtushwa na mauaji zaidi ya raia kutokana na mapigano ya mapema wiki hii mjini Mogadishu. Watu zaidi ya 30 wameuawa, wengi ni raia, hasa wanawake na watoto.

Taarifa walizozipata UNHCR kutoka Moghadishu zinasema hospitali mjini humo zinashindwa kumudu idadi kubwa ya majeruhi. UNHCR imerejea wito wake kwa pande zinazohusika na mapigano Somalia kuepuka kulenga maeneo ya raia na maeneo yenye watu wengi Mogadishu ambayo yanawakimbizi wa ndani laki tatu.