Skip to main content

UNHCR yapongeza Tanzania kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi

UNHCR yapongeza Tanzania kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi

Kamishina Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR, Antonio Guterres amepongeza hatua ya serikali ya Tanzania kuwapa uraia wakimbizi wa Burundi.

Guterres akiwa eneo la Katumba magharibi mwa Tanzania ,waziri wa mambo ya ndani wa nchi hiyo Lawrence Masha alitaja orodha ya kwanza rasmi ya wakimbizi wa Burundi waliopewa uraia ambao wengi wamekuwepo Tanzania tangu mwaka 1972.

Bwana Guterres ameitaka jumuiya ya kimataifa kutambua na kuithamini hatua hiyo ya Tanzania na amewataka wahisani kusaidia shughuli ya kuwarejesha katika maisha ya kawaida wakimbizi hao.