Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban akaribisha maafikiano ya kuondoka Kyrgystan aliyekuwa Rais wa nchi hiyo

Ban akaribisha maafikiano ya kuondoka Kyrgystan aliyekuwa Rais wa nchi hiyo

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon ameunga mkono mpango uliomuwezesha Rais Kurmanbek Bakiyev kuondoka Kyrgyzstan.

Katika taarifa yake iliyotolewa leo Ban anaamini kwamba hii ni hatua muhimu kuelekea amani, taifa thabiti, matarajio na maendeleo ya nchi yanayofuta misingi ya demokrasia na utawala bora. Mgogoro nchini Kyrgyzstan ulianza wiki iliyopita kwa maandamano kwenye mji wa kaskazini magharibi wa Talas na kisha kuasambaa hadi mji mkuu Bishkek na hatimaye kuufanya upinzani kuunda serikali ya mpito.

Jana Jumatano Rais huyo wa zamani Bakiyev alisema kwamba alikuwa tayari kuondoka nchini humo endapo serikali ya mpito itamuhakikishia usalama wake na wa familia yake. Serikali hiyo ya muda ya Kyrgyzstan imefanya mipango ya rais huyo aliyepinduliwa kuondoka nchini. Ban amesema Umoja wa Mataifa na washirika wake wako tayari kufanya kazi na uongozi wa Bishkek kwa niaba ya watu wa Kyrgyzstan.