Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

UNAMID inasema wanajeshi wake waliotoweka huenda wametekwa nyara

UNAMID inasema wanajeshi wake waliotoweka huenda wametekwa nyara

Mpango wa kulinda amani wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika kwenye jimbo la Darfur Sudan UNAMID leo umesema wanajeshi wake wane waliotoweka huenda wametekwa nyara.

Mwakilishi maalumu wa UNAMID Dr Ibrahim Gambari amesema licha ya juhudi zote wanazofanya wanajeshi hao na gari lao bado hawajapatikana. Amesema wasiwasi wao hivi sasa ni kwamba huenda watu hao wametekwa. Amesema tofauti na ripoti za vyombo vya habari hakuna mtu yeyote aliyewasiliana nao au kundi lolote, au kupata madai yoyote ya kikombozi.

Lakini gazeti la kila siku mjini Khartoum limearifu kwamba kundi la waasi la People's Struggle Movement limedai kuwateka wanajeshi hao wanne. Na msemaji wa kundi hilo amesema wanadai kikombozi cha pauni bilioni moja za Sudan sawa na dola za Marekani milioni 447.7.