Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Idadi ya waliokufa katika tetemeko uchina inazidi kuongezeka

Idadi ya waliokufa katika tetemeko uchina inazidi kuongezeka

Idadi ya watu waliokufa katika tetemeko la ardhi kwenye jimbo la Qinghai jana asubuhi sasa imefikia zaidi ya 600.

Watu wengine zaidi ya 10,000 wamejeruhiwa katika tetemeko hilo lililosambaratisha majengo mengi, miundombinu na njia za mawasiliano.

Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon amesema Umoja wa Mataifa uko tayari kutoa msaada utakaohitajika kuisaidia Uchina katika wakati huu mgumu.Nalo shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia watoto UNICEF linasema liko tayari kwa ajili ya msaada wowote utakaohitajika.

Shughuli za uokozi zinaendelea na chama cha msalaba mwekundu nchini humo kikitoa msaada. Francis Markus wa chama hicho anafafanua waliofanya hadi sasa