Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

FAO imechapisha mpango mpya kuhusu masuala ya jinsia katika kilimo

FAO imechapisha mpango mpya kuhusu masuala ya jinsia katika kilimo

Katika juhudi za kukabiliana na njaa shirika la Umoja wa Mataifa la chakula na kilimo FAO limezindua mpango wa kupata taarifa za usahihi za tofauti zilizopo baiana ya wanawake na wanaume kwenye sekta ya kilimo.

Mtandao huo mpya uitwao Agri-Gender database ambao umeanzishwa kutokana na ombi la tume ya Afrika ya takwimu za kilimo utatoa muongozo wa hatua kwa hatua wa jinsi gani ya kukusanya takwimu tofauti za kijinsia katika kilimo. Mtandao huo utajumuisha masuala kama idadi ya watu walio katika kilimo na nyumbani, uwezo wa kupata rasilimali, uzalishaji na mazao yake, kazi wanayofanya na muda wanaotumia na pia yanakopelekwa mazao. Pia itajumuisha mapato na matumizi, uanachama katika mashirika ya kilimo na dalili za upungufu wa chakula na umasikini.

FAO imebaini kwamba mchango wa wanawake na wasichana katika uzalishaji wa kilimo mara nyingi haupewi uzito mkubwa kwa sababu takwimu ya kinachozalishwa huchukuliwa kwenye kumbukumbu za wamiliki wa ardhi ambao wengi ni wanaume.