Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Tanzania kuendelea na mchakato wa kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Burundi

Tanzania kuendelea na mchakato wa kuwarejesha nyumbani wakimbizi wa Burundi

Nchi ya Tanzania iliyoko Afrika ya Mashariki inahifadhi wakimbizi karibu laki moja wengi wao wakiwa kutoka Burundi na Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Mkuu wa shirika la Umoja wa Mataifa la kuhudumia wakimbizi UNHCR Bwana Antonio Guterres amekuwa ziarani nchini humo kwa juma zia ambako amekutana na baadhi ya wakimbizi kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na Burundi walioko mkoani Kigoma. Pia ametatathimini mchakato wa kuwapa uraia Warundi laki moja na sitini ambao wamekuwemo nchini humo tangu mwanzoni mwa miaka ya 1070.

Hata hivyo Warundi zaidi ya laki tano ambao waliomba ukimbizi katika miaka ya 1990, idadi kubwa walirejea nyumbani kati ya mwaka 2002 na mwaka jana. Msemaji wa wizara ya mambo ya ndani wa Tanzania Isaac Nantanga amezungumza na mwandishi wa radio washirika wetu ya TBC1 na kumueleza hali ya sasa ya shughuli ya kurejea nyumbani kwa wakimbizi hao.