Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Ban Ki-moon ametoa wito kwa nchi kuimarisha afya ya mama na mtoto

Ban Ki-moon ametoa wito kwa nchi kuimarisha afya ya mama na mtoto

Ikiwa imesalia miaka mitano tuu kabla ya kufikia 2015 kilele cha kutimiza malengo ya maendeleo ya milenia Katibu Mkuu wa UM ametoa wito wa kuongezwa juhudi.

Bwana akizungumza na waandishi wa habari hii leo amezitaka nchi zote kuchukua hatua ili kushughulikia lengo la tano la milenia ambalo limekuwa likisuasua la afya ya mama na mtoto. wengine waliozungumza katika mkutano huo ni Rais Jakaya Kikwete wa Tanzania.

Ban amesema wanawake wanatimiza malengo na sio ya kuzaa watoto tuu. Na kama nasi tutawatimizia, tutabadili dunia kwa mambo mazuri. Katika malengo yote ya milenia la afya ya mama na mtoto ndio lililobaki nyuma na hilo ndio kitovu cha yote.

Ameongeza kuwa wakati kwingineko vifo vya watoto vinapungua maelfu ya wanawake wanaendelea kupoteza maisha kila mwaka wakati wa ujauzito au wakati wa kujifungua na wengine milioni 10 hadi 15 wanapata matatizo makubwa. Ban Ki-moon amezindua mpango maalumu ambao amesema utamuweka mama na mtoto katika kipaumbele.