Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Hatua zimepigwa kuingiza vifaa vya ujenzi Gaza lakini hazitoshi

Hatua zimepigwa kuingiza vifaa vya ujenzi Gaza lakini hazitoshi

Mkuu wa masuala ya kisiasa wa Umoja wa Mataifa Lynn Pascoe katika taarifa yake ya kila mwezi kwenye baraza la usalama kuhusu masuala ya mashariki ya kati amesema hatua zimepigwa kuingiza vifaa vya ujenzi Gaza.

Amesema kutokana na Israel kuruhusu kuingia kwa changarawe na simenti sasa ujenzi umeanza wa mtaro wa maji machafu na miradi mingine iliyoidhinishwa ukiwemo wa ujenzi wa nyumba unaotarajiwa kuanza hivi karibuni.

Bwana Pascoe amesema kazi katika miradi iliyoidhinishwa ni mwanzo wa kiasi tuu cha kinachohitajika kufanywa Gaza baada ya zaidi ya mwaka mmoja wa uharibifu uliofanywa na operesheni za jeshi la Israel.