Simu za mkononi zilizoko India ni nyingi kuliko idadi ya vyoo:UM

14 Aprili 2010

Mapendekezo yaliyotolewa leo na chuo kikuu cha Umoja wa Mataifa ya kupunguza idadi ya watu wasio na vyoo yanaonyesha, India nchi ambayo ni ya pili kwa idadi kubwa ya watu duniani wana simu za mkononi nyingi kuliko vyoo.

Zafar Adeel mkurugenzi wa chuo kikuu cha Umoja wa Mataifa cha maji, mazingira na afya amesema inasikitisha kuona kwamba India nchi ambayo ina utajiri wa kutosha nusu ya watu wake wanasimu za mkononi lakini hawawezi kumudu huduma muhimu ya vyoo.

India ina simu za mkononi milioni 545 ambazo zinatosheleza asilimia 45 ya watu wote ,lakini ni watu milioni 366 au asilimia 31 tuu ya watu wote ndio wanaomudu huduma bora ya vyoo. Mapendekezo ya leo ni kuchagiza kasi ya kufikia malengo ya milenia ya kuwa na uwiano wa watu ambao hawana maji safi na huduma ya vyoo.

 

♦ Kutembelea ukurasa maalum wa COP26 bofya  hapa.
♦ Iwapo ungependa kupokea taarifa kutoka UN News Kiswahili kila wakati zinapochapishwa jisajili  hapa.
♦ Pia unaweza kupakua apu ili kusikiliza matangazo yetu wakati wowote popote ulipo.
♦ Tembelea pia chaneli yetu ya Youtube na pia Soundcloud na Twitter