Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Baraza la usalama kuzuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni wa wiki

Baraza la usalama kuzuru Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo mwishoni wa wiki

Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa linatuma ujumbe nchini Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo kuanzia Jumamosi ijayo.

Kwa mujibu wa balozi wa Ufaransa kwenye Umoja wa Mataifa Gerard Araud ujumbe huo utakuwa na wakilishi wa kudumu saba ,manaibu wawakilishi wa kudumu sita na washauri wawili.

Ujumbe huo utajadiliana na serikali ya Congo na pande zingine husika maandalizi ya jukumu la mpango wa Umoja wa Mataifa wa kulinda amani nchini humo MONUC.

Balozi Araud amesema ujumbe huo pia utajadili hatma ya uwepo wa Umoja wa Mataifa nchini Congo. Katika ripoti yake ya karibuni kuhusu Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Katibu Mkuu Ban Ki-moon amependekeza kupunguza wanajeshi wa kulinda amani elfu mbili kati ya 20,000 waliko nchini humo ifikapo mwezi Juni.Ujumbe huo utakuwa mjini Kinshasa kwa siku mbili kabla ya kurejea New York Jumanne ijayo.