Mtazamo wa Kimataifa Habari za kiutu

Mratibu wa masuala ya kibinadamu ahofia usalama wa watu Mogadishu

Mratibu wa masuala ya kibinadamu ahofia usalama wa watu Mogadishu

Mratibu wa Umoja wa Mataifa kwa masuala ya kibinadamu nchini Somalia ameelezea hofu yake kuhusu hali ya raia nchini Somalia kutokana na mapigano yanayoendelea mjini Moghadishu.

Ameongeza kuwa mfumo wa mapigano yenyewe ndio unaleta shida kwani makundi ya wanamgambo wanatumia mabomu na makombora na majeshi ya serikali yanajibu, sio mashambulizi yanayolenga wanajeshi hivyo yanaleta athari kwa wahusika na wasiohusika. Bwana Bowden amezitaka pande zinazohusika kuwajali raia kwani amesema ni vigumu kwa mashirika ya misaada kwa sasa kupeleka mahitaji muhimu kama maji na chakula kwa wakimbizi.